Wednesday, July 24, 2013


NA ZAINAB IDDY

CHAMA cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam (DAAA), kimewataka wazazi na walimu wa shule za msingi na sekondari kutoa nafasi kwa wanafunzi kwenda kushiriki mchujo wa kutafuta timu ya mkoa, ambayo itawashiriki michuano ya taifa ya mchezo huo.

Mashindano hayo yatakayofanyika mkoani Morogoro Agosti 23na 24, yatashirikisha mikoa yote ya Tanzania bara.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa DAAA, Kapteni mstaafu Lucas Nkungu alisema ili kuweza kupata timu bora itakayowakilisha mkoa, unahitaji ushirikiano mkubwa kutoka kwa wadau ambao ni walimu na wazazi.

“Maandalizi katika shule zote yameshaanza na wameanza kufanya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mashindano hayo na sisi tumejipanga kuhakikisha yanafanyika kama tulivyokusudia,” alisema Nkungu.

Alisema wameamua kuchukua timu za shule za msingi na sekondari, kuwashindanisha kwa lengo la kupata vijana wadogo kuwa na hazina kubwa za mchezo huo siku zijazo.

0 comments:

Post a Comment