Wednesday, July 24, 2013


 NA NYEMO MALECELA

MWANARIADHA maarufu nchini, Zakia Mrisho amejiondoa kwenye orodha ya wanariadha watakaoshiriki kwenye michuano ya Dunia itakayoanza kutimua vumbi Agosti 10 mwaka huu jijini Moscow, Urusi.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui, nyota huyo alikuwa ashiriki kwenye mbio za mita 5000, huku akitaja sababu kubwa za kujitoa kwake ni kutokana na ugonjwa.

Wakati huo huo, idadi ya Watanzania watakaoshiriki michuano hiyo imeendelea kupungua baada ya mwanariadha mwingine mkongwe, Samson Ramdhani kujitoa kutokana na umri kuwa mkubwa.

Kufuatia wanariadha hao mashuhuri kutoshiriki michuano hiyo ya Dunia, sasa Tanzania itawakilishwa na wakimbiaji wawili tu, ambao ni Faustine Musa na Msenduki Mohamed ambao wote watakimbia mbio ndefu za umbali wa kilometa 42.

0 comments:

Post a Comment