Wednesday, July 24, 2013


OLIPA ASSA

NYOTA wa muziki wa Injili Tanzania, Kabula George, anatarajiwa kupanda jukwaani jijini Mbeya kwenye muendelezo wa matamasha yake nchi nzima.

Akizungumza na DIMBA jijini Dar es Salaam, Kabula amesema kuwa tamasha hilo linatarajiwa kufanyika Agosti 4 mwaka huu, huku akisindikizwa na waimbaji wengine wa muziki huo Tanzania.

“Pamoja na mimi kuimba, lakini watakuwepo waimbaji wengine kutoka maeneo mengine ya Tanzania ikiwemo Mbeya kwenyewe ambao wanafanya vizuri kwenye muziki huo kwa sasa.

“Wengine ni pamoja na Ambale Chapanyota, Christina Shusho, Dotnata pamoja na pacha wake ambao kwa sasa wanaimba Muziki wa Injili, pia zitakuwepo kwaya nyingine kutoka Mkoa wa Mbeya.

“Tumejaribu kuangalia na kuona kwamba tuweke kiingilio cha chini ambacho ni shilingi 2000 kwa mkubwa na watoto ni shilingi 1000, ili kila mkazi wa Jiji la Mbeya na maeneo jirani wasiikose siku hiyo,” alisema Kabula anayetamba na albamu yake ya Nitang’ara tu.

0 comments:

Post a Comment