Wednesday, July 24, 2013


NA NYEMO MALECELA

TIMU ya Polisi Moro iliyoshuka daraja msimu uliopita, imetoa wachezaji tisa watakaounda timu ya kijeshi itakayoshiriki michuano ya SADEC itakayofanyika nchini Namibia.

Ofisa Habari wa Polisi Moro, Clement Bazzo ameliambia DIMBA kuwa wachezaji hao ambao wamejiunga na kambi ya timu ya Polisi ya taifa jijini Dar es Salaam, jana wameongezewa mkataba wa mwaka mmoja.

Aliwataja wachezaji hao kuwa ni John Tamba, Nahodha Bakari, Salimin Kisi, Kondo Salumu, Mokili Rambo, Deta Tomasi, Nochorous Kabipe, Imani Mapunda na Tiba Abdalah.

“Wachezaji hao wameungana na wengine kutoka timu za Polisi za mikoa Tanzania na kuunda timu moja ya taifa ya Polisi itakayoshiriki michuano hiyo ya majeshi na itakapomalizika watarejea kwenye kikosi chao,” alisema Bazzo.

0 comments:

Post a Comment